Azam FC
imeingia fainali ya Kombe la Kagame, inakipiga na Gor Mahia ya Kenya kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Ni fainali ya
pili ya Azam FC ndani ya miaka mitatu tu. Lakini inasubiri rekodi ya aina yake
kwa kuwa hadi inafika hapo, haijafungwa hata bao moja katika michuano ya mwaka
huu.
Hata kama
itafungwa bao moja au mawili leo, itaondoka na rekodi ya kuwa na difensi bora
kabisa.
Lakini ikibeba
kombe bila kufungwa, basi itakuwa imeweka rekodi ya kuwa bingwa wa aina yake
mwenye safu ya ulinzi ya chuma.
Kwa Watanzania,
furaha ni kuona Azam FC inatwaa kombe na kulibakiza nyumbani.
KILA LA KHERI
AZAM FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment