Timu ya Neckarsulmer anayochezea
Mtanzania, Emily Mgeta imeingia raundi
ya pili ya Kombe la Wfv-Verbandspokal.
Kombe hilo
linaloshirikisha timu zote za juu za jimbo la Wütternberg nchini Ujerumani ni
kati ya michuano migumu.
Neckarsulmer imeshinda
mabao 6-0 dhidi ya Tsv Schwaikheim na kama itashinda mchezo ujao, itaingia
katika nafasi ya kucheza michuano DFB Polka sawa na Kombe la FA nchini England.
“Kwa kweli ni faraja
sana, mechi iliyopita tulishinda tano, hii tumeshinda sita. Lengo ni kufikia
kucheza Kombe la FA,” alisema Mugeta aliyewahi kukipiga Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment