Mshambuliaji aliyeonekana hafai Yanga, Said
Bahanuzi, amesema amezaliwa upya na anayebisha akamtazame akichezea kikosi
hicho.
Bahanuzi alitolewa kwa mkopo na Yanga kwenda
Polisi Moro ambayo imeshuka daraja msimu uliopita, hivyo kuamua kuachana naye
baada ya kubakiza mkataba wa mwaka mmoja.
Bahanuzi
amesema amejipanga kuitumikia timu yake mpya kwa nguvu zote kuhakikisha
inafanya vizuri katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
“Naomba uzima niweze kuisaidia timu yangu kwani
ninachotakiwa kukifanya kwa upande wangu ni kuhakikisha najituma kwa nguvu zote
ili kufanya vyema.
“Sasa nimezaliwa upya na nafanya vizuri
mazoezini, hata katika mechi nitakuwa vizuri, watu wataona yale makali yangu
yaliyopotea,” alisema Bahanuzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment