Dirisha la Usajili kwa klabu za Ligi Kuu (VPL), Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (RCL) linatarajiwa kufungwa
tarehe 06 Agosti, 2015.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
linavikumbusha vilabu vyote kufanya usajili wa wachezaji wao mapema kabla ya
kufungwa kwa dirisha hilo, ili kuondokana na usumbufu wa kufanya usajili dakika
za mwisho.
Pindi dirisha hilo litakapofungwa Agosti 06, hakuna
klabu au timu yoyote itakayoweza kufanya tena usajili wake, hivyo ni vyema
vilabu vitahakikisha vinamaliza mausala ya usajili mapema kabla ya siku ya
mwisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment