Kocha Mwingereza, Dylan Kerr amesema haoni
sababu ya Simba kurejea katika kambi mjini Zanzibar.
Kerr amesema hayo baada ya uongozi wa Simba
kutaka kikosi hicho kirejee kuweka kambi Zanzibar baada aya kocha huyo kukataa
ile kambi nchini Oman.
Baada ya kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza
chini yake kwenye uwanja huo, Kerr raia wa Uingereza, amesema haoni haja ya
kurudi tena Zanzibar kwani sehemu wanayotumia sasa kwa mazoezi ni nzuri.
“Nilikuwa sijui kama kuna uwanja mzuri kama
huu hapa Dar es Salaam, ndiyo maana nilitaka turudi Zanzibar baada ya safari
yetu ya Oman kukwama lakini kwa sasa hakuna sababu yoyote ya kurudi huko,”
alisema Kerr.
Simba itabidi ‘ijipige’ kidogo mfukoni kwani
ili kuutumia uwanja huo inalazimika kulipa Sh 300,000 kila siku kwa ajili ya
mazoezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment