Wasanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Saleh
Kiba ‘Aki Kiba’ kesho Jumapili wanatarajiwa kutumbuiza katika uzinduzi wa
kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Diamond na Ali Kiba ni sehemu ya wasanii wengi
wa muziki na wale wa filamu watakaotoa burudani kwenye uzinduzi huo
unaotarajiwa kufanyika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kitendo cha Ali Kiba na Diamond kupanda jukwaa
moja ni nadra kutokea kutokana na upinzani uliopo kati yao, hiyo watu
watakaofika kwenye uzinduzi huo watapata burudani ya bure ya aina yake.
Mbali na kutamba na nyimbo nzuri kwa kila mmoja
wao, kumekuwa na upinzani mkali kuhusu msanii mkali wa kutawala jukwaa, hivyo
wawili hao wanatarajiwa kutoa burudani ya kiwango cha juu ili kuendelea
kuthibitisha ubora wao.
Magufuli amepata nafasi hiyo baada ya kupita
katika mchujo wa watangaza nia zaidi ya 40 waliojitokeza ndani ya CCM. Uchaguzi
Mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment