Mshambuliaji
mpya wa Chelsea, Radamel Falcao amesema wala hana presha.
Falcao
ambaye amejiunga na Chelsea akitokea AS Monaco iliyokuwa imempeleka Man United
kwa mkopo, amesema ana imani mvua ya mabao kutoka kwake inakuja.
“Kweli
sikuwa na msimu mzuri Man United, lakini sasa nina nafasi ya kuonyesha
ninaweza.
“Najua
nitafunga, najua mabao yatapatikana na sipaswi kuwa na presha,” alisisitiza.
Mambo
yake hayakwenda vizuri akiwa na Man United, hali inayoonyesha kwamba itampa
presha zaidi akiwa Chelsea ambayo imemnunua kabisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment