Dereva maarufu wa magari ya langalanga, aina ya Mercedes,
Lewis Hamilton sasa kuna taarifa anajiachia na mwanadada Rihanna.
Rihanna ambaye ni mwanamuziki wa pop, asili yake ni Barbados
ambako sasa yeye na Hamilton wako huko.
Taarifa zinaeleza wawili hao wamekuwa wakikutana na kuendeleza
‘mambo’ yao.
Hamilton yuko Barbados katika michuano ya langalanga na
Rihanna ametua huko kwa ajili ya zile sherehe maarufu kama inavyokuwa Carnival
nchini Brazil.
Hivyo wamepata nafasi ya ‘kujipa raha’ wenyewe ingawa hakuna
mmoja wao aliyepata nafasi ya kulizungumzia hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment