Kocha wa Bayern Munich
Pep Guardiola amecharuka na kama si watu kuwahi, angeweza kuzichapa na kiungo
wa AC Milan, mkongwe Nigel De Jong.
Pep alikuwa akimlalamikia
kiungo huyo kumchezea rafu kiungo wake kinda Joshua Kimmich wakati timu hizo
zilipokutana katika mechi ya michuano ya Audi Cup mjini Munich.
Kocha huyo alianza kumpa
De Jong maneno makali, alimsisitiza si mtu makini aliyeshindwa hata kumuona
kiungo huyo ni kinda ambaye anatakiwa kupewa moyo badala kuonyeshwa soka ni
mchezo wa kikatili.
De Jong alicharuka baada
ya Pep kukumbushia ile faulo yake ya fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010
alipomrukia tumboni Xabi Alonso ambaye sasa anakipiga Bayern Munich.
Hali hiyo ilimuudhi sana
De Jong ambaye alitaka kumvaa Pep lakini wakaamuliwa wakati wakiingia vyumbani. Bayern ilishinda mechi hiyo kwa mabao 3-0.
KIMMICH (KULIA) KABLA YA KUUMIA SIKU HIYO. |
FAINALI KOMBE LA DUNIA 2010 |
0 COMMENTS:
Post a Comment