SHERMAN AKIWA KATIKA SARE ZA MPUMALANGA |
Wakala wa mshambuliaji mpya wa
Mpumalanga Balack Aces, amesema ana imani kubwa na mshambuliaji huyo kufanya
vema.
Gibby Kalule amesema Sherman ana
uwezo mkubwa, kinachotakiwa ni kumpa muda tu.
“Ligi ya Afrika Kusini ni ngumu na
kubwa, Sherman ni mchezaji mzuri anayejitambua. Kinachotakiwa hapa ni muda tu.
“Kama atapewa muda, nina imani
atafanya vizuri tu. Ni mtu anayeweza ushindani,” alisema.
Sherman raia wa Liberia amejiunga na
Aces akitokea Yanga ambayo ameichezea kwa msimu mmoja tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment