August 1, 2015

DUSAN (WA PILI KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA MWINYI KAZIMOTO. KULIA NI BOSI WAKE DYLAN KERR NA MSAIDIZI, SELEMANI MATOLA.
Kocha wa viungo wa Simba, Dusan Momcilovic, ametamba kuwa ana uhakika zaidi ya asilimia 90 kikosi chao kitatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao kutokana na mazoezi wanayofanya.

Momcilovic, raia wa Serbia, maarufu kama Dule, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kama wachezaji wa Simba watafuata maelekezo yake kuhusu utimamu wa miili yao, hakuna klabu itakayowababaisha.

Dule, huku akiziponda timu ambazo hazina makocha wa viungo wenye utaalam, ikiwemo Yanga, alisema mambo yakiendelea kama walivyopanga, basi Simba haina kizuizi cha kutotwaa ubingwa.

“Mwanzo wachezaji hawakuwa fiti wakishindwa hata kumaliza programu moja, lakini sasa wana uwezo wa kucheza zaidi ya mechi moja bila kuchoka. Naamini tunaweza kufanya vema iwapo tu wachezaji wataendelea kufuata programu zangu hadi mwisho wa msimu.

“Hivi kama unakuwa na timu ambayo wachezaji wake wana kasi, nguvu na stamina kubwa na wana uwezo wa kucheza zaidi ya mechi moja, bila kuchoka kwa nini usichukue ubingwa? Basi hesabu Simba bingwa msimu ujao,” alisema Dule.

Simba inatarajiwa kumaliza kambi yake ya Zanzibar katikati ya wiki ijayo ili kushiriki shughuli za wiki yake ya maadhimisho ya Simba Day itakayofanyika Jumamosi ijayo ya Agosti 8, mwaka huu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic