August 1, 2015


MKWASA.
Serikali imekataa kumlipa mshahara kocha wa muda wa Taifa Stars, Charles Mkwasa kwa kisingizio kuwa fedha hizo ni maalum kwa wageni tu, tofauti na maombi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Wakati TFF ikimpa kazi Mkwasa ya kuinoa Taifa Stars, rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi alisema angeiomba serikali imlipe kocha huyo stahiki zote kama ilivyokuwa ikifanya kwa makocha wageni.

Taarifa zimeeleza Serikali imegoma kumlipa Mkwasa na badala yake TFF imekuwa ikimlipa posho kocha huyo kama kifuta jasho.

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa kutoa ufafanuzi wa sakata hilo, alisema: “Ni kweli hakuna malipo ya mshahara wa Mkwasa yaliyofanywa na serikali, ila sisi kama TFF tulimlipa posho tu kwa kazi yake. Tupeni muda tunalifanyia kazi jambo hili.”

Kuhusiana na malipo ya aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ambaye bado yupo nchini, Mwesigwa alisema: “Nooij hatudai chochote, tumeshamalizana naye na kama yupo nchini ni kwa mapenzi yake tu.”
Hivi karibuni TFF katika maazimio ya kamati yake ya utendaji ilikubaliana kusitisha mkataba wa Nooij na nafasi yake kupewa Mkwasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic