Mshambuliaji mpya wa Yanga, Donald Ngoma amesema ana imani
kubwa na kikosi chao cha Yanga.
Ngoma amesema presha kubwa aliyoipata kwenye michuano ya Kagame
hasa baada ya kupata kadi nyekundu, imemfunza mengi kuhusiana na soka la
Tanzania na ukanda wote wa Afrika Mashariki.
“Presha ililkuwa kubwa sana, niliona siku haziende. Lakini nimejifunza
jambo na Yanga ina kikosi bora kabisa.
“Mimi nina imani kubwa na kikosi chetu kitafanya kazi nzuri tu
kwa kuwa kuna ushirikiano mzuri, watu wanajituma na wanataka kushinda.
“Kama tulifanya makosa kwenye Kagame, basi tunaitumia nafasi
hiyo kwa kuyarekebisha,” alisema Ngoma.
Ngoma raia wa Zimbabwe, alilambwa kadi nyekundu katika mechi
ya kwanza tu ya michuano ya Kagame wakicheza dhidi ya Gor Mahia na Yanga
ikalala kwa mabao 2-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment