Nyota wa Chelsea, kiungo John Obi Mikel,
amemtibua Kocha wa Nigeria, Sunday Oliseh kwa kumuonyesha dharau na ameondolewa
katika kikosi kitakachoivaa Taifa Stars mwezi ujao.
Septemba 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, Taifa Stars itacheza na Nigeria ‘Super Eagles’ katika
mchezo wa Kundi G kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika 2017.
Oliseh alisema amemuondoa kikosini Obi kutokana
na kitendo chake cha kutowasiliana naye na hata alipofuatwa jijini London,
England hakuonyesha kujali.
“Mwenzake Victor Moses wanayecheza naye
Chelsea, nilipokwenda London nilikutana naye na akaniambia ana majeraha kidogo,
huyu nilimuelewa. Lakini Obi nilimpigia simu hakupokea, nikamtumia ujumbe mfupi
(SMS), hakujibu.
“Hatutaki kuonekana tunamtegemea mchezaji mmoja
katika timu, kikosi kina wachezai 11 ambao wakishirikiana ndiyo timu inapata
ushindi, siwezi kuzungumzia zaidi ya hapa,” alisema Oliseh ambaye ni nyota wa
zamani wa Super Eagles.
0 COMMENTS:
Post a Comment