Simba imeamua kuachana na straika Kevin
Ndayisenga baada ya kutokubaliana na sharti alilotaka kulipwa dola 100 (Sh
207,610) kwa kila bao atakalofunga.
Awali viongozi wa Simba walikuwa wanataka kuona
uwezo wa Ndayisenga raia wa Burundi kwanza halafu ndiyo wakubaliane vipengele
vya mkataba baada ya kuridhika naye.
Kama zali, Ndayisenga akafanya vizuri katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya URA kwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao
2-1 iliyoupata Simba wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Straika huyo pia alitaka alipwe dau la usajili
dola 30,000 (Sh milioni 62) na wakala wake alipwe dola 15,000 (Sh milioni 31)
na mshahara wa dola 1,000 (Sh milioni 2).
Bosi mmoja wa Kamati ya Usajili ya Simba,
amesema kutokana na mahitaji hayo ya Ndayisenga
wameshindwa kumudu na wameachana naye tayari.
“Ndayisenga anataka kila akifunga tumpe dola
100, tumeshindwana naye ndiyo maana tumemleta Papa Amadou Niang kutoka
Senegal,” alisema bosi huyo mwenye sauti kuhusu mambo ya usajili Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment