Na Said Mohammed, Zanzibar
Simba imeitwanga
Jang’ombe Boys ya Zanzibar kwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa
leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Mabao ya Simba
yamefungwa na Elius Maguri, dakika ya 14, Michael Mgimwa dakika ya 17 na Samir
Omar katika dakika ya 81 na Kocha Dylan Kerr amesema angalau.
“Mechi ilikuwa nzuri,
lakini kuna mambo kadhaa tunapaswa kubadilisha kama utumiaji wa nafasi
tulizozipata.
“Tumetengeneza nyingi
zaidi lakini tumefunga chache, ni vizuri kutumia nafasi kwa zaidi ya asilimia
70, sisi hatukufanya hivyo,” alisema Kerr raia wa Uingereza.
Hii ni mechi ya nne
Simba inashinda mfululizo ikiwa visiwani hapa. Ilianza na kombaini ya Zanzibar
2-1, ikaituliza Black Sailors 4-0 na Polisi 2-0. Leo imemtungua mtu 3-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment