Simba imeamua kuachana na mshambuliaji Laudit Mavugo.
Simba imefikia uamuzi huo baada ya kuona kuna hali ya
sintofahamu iliyopitiliza.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba, zimeeleza Mavugo ana
mkataba na mmoja wa viongozi wa Vital’O ambaye amewasumbua kabla ya kufikia
naye makubaliano.
“Lakini baada ya kumalizana na kiongozi huyo, viongozi
walioingia madarakani nao wamekuja na mambo mapya.
“Sasa limekuwa jambo moja linazungumzwa kila wakati na
haliishi, uongozi umeamua kuachana naye,” kilieleza chanzo.
Kutokakana na hali hiyo, Simba tayari imeanza juhudi za kupata
mshambuliaji wa kati.
Hata hivyo, bado inaonekana kama mkongwe Mussa Mgosi na Hamis Kiiza
wanaweza kuingoza safu hiyo ya ushambuliaji vizuri wakishirikiana na vijana wengine kama Ibrahim Ajibu, Elius
Maguri na wengine wanaochipukia.
0 COMMENTS:
Post a Comment