SHERMAN AKIWA KATIKA SARE YA MPUMALANGA BLACK ACES MARA TU BAADA YA KUSAINI MKATABA LEO ASUBUHI. |
Kpah Sherman amekamilisha usajili wa
miaka mitatu katika klabu ya Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga
raia wa Liberia aliyezaliwa miaka 23 iliyopita tayari anaonekana akiwa katika
mtandao wa timu hiyo ukithibitisha kujiunga na klabu yao.
Taarifa zinaeleza ameuzwa dola
150,000, hata hivyo zimekuwa hazina uhakika kwa kuwa Amazayon na Yanga wameficha
kuhusiana na uhamisho huo.
Mwenyekiti wa klabu hiyo maarufu kama
Amazayon amejivunia kufanikiwa kumnasa Sherman akimfananisha na George Weah.
Mario Morfou
amesema:
“Ni
mchezaji mzuri anayeweza kutusaidia katika Ligi ya PSL. Tunaamini atashirikiana
vizuri sana na Collins Mbesuma kuhakikisha tunafanya vema.
“Ni
mshambuliaji aliyechukua ubingwa katika nchi mbili, bado kidogo amfikie George
Weah ambaye ni gwiji wa Liberia, Afrika na dunia nzima ambaye alichukua mara
tatu.
Sherman
ambaye alijiunga na Yanga akitokea
katika klabu Centikaya Turk S.K.
hakuonekana kuwa msaada mkubwa kama alivyoonyesha awali katika mechi ya kumpima
kabla ya kujiunga.
Aliichezea Yanga mechi ya kwanza dhidi ya Simba ikiwa ni siku moja tu baada ya kutua nchini, akaonyesha uwezo mkubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment