Je, unajua kikosi cha kuwa wachezaji saba raia wa Tanzania
walikuwa katika kikosi cha Azam FC kilichofanikiwa kutwaa ubingwa wa Kagame
dhidi ya Gor Mahia?
Wachezaji hao ni kipa Aishi Manula, John Bocco aliyekuwa
nahodha, Himid Mao, Aggrey Moris, Said Morad, Ame Ally, Shomari Kapombe na Shah Farid Mussa.
Wakati wageni watatu walioanza walitokea katika nchi mbili tu
za Rwanda na Ivory Coast.
Wageni hao walikuwa ni Jean Baptiste ‘Mugiraneza’ kutoka
Rwanda pamoja na Serge Wawa na Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast.
Katika mechi hiyo ambayo Azam FC walishinda kwa mabao 2-0, moja lilifungwa na mwenyeji Bocco na moja likafungwa na mgeni Kipre hali inayoonyesha kiasi gani wageni na wenyeji walivyo na mchango mkubwa katika kikosi hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment