MWALALA WAKATI AKIWA YANGA... |
Ben Mwalala ambaye alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, sasa
amewaonya makocha kuachana na tabia za kulaumu waamuzi.
Mwalala ambaye sasa ni mwamuzi wa Nzoia United ya kwao Kenya,
amesema makocha wanapaswa kupunguza kulia na waamuzi.
“Unajua nimeona hii tabia nikiwa Tanzania, pia naiona sasa nikiwa
hapa nafundisha. Sidhani kama ni sahihi kila baada ya mechi kocha kulia na
mwamuzi.
“Vizuri kwa timu kutafuta nafasi na mwisho kufunga kwa faida ya
timu. Lakini si kupiga kelele na waamuzi muda wote,” alisema Mwalala.
Mwalala alikuwa mmoja wa washambuliaji wenye kasi kubwa wakati
akiitumikia Yanga.
Baadaye aliamua kujiendeleza kwa kusoma ukocha kabla ya kuanza
kazi ya kufundisha akianzia hapa nchini kabla ya kurejea kwao Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment