MANARA |
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema uongozi wa Yanga hautapata
nafasi ya kuzungumza kabisa.
Uongozi wa Yanga umeamua ‘kuvikaushia’ vyombo vya habari kwa madai
kwamba wanataka kuzungumza baada ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Simba.
“Wanakutana na wafalme wao ndiyo maana wameamua kukaa kimya.
Watakaa kimya sana na hawatakuwa na nafasi ya kuzungumza tena.
“Watakuwa na kipi cha kuzungumza wakati watakuwa wamefungwa. Acha waendelee
kukaa kimya,” alisema Manara.
Mashabiki wengi wa Yanga wamekuwa wakilalamika kuona Yanga wakiwa
kimya bila ya kuzungumza lolote.
Baadhi wamekuwa wakisema huenda Yanga wanataka kutosema lolotea
kwa kuwa wanajua Simba ni wenyeji.
Badala yake, vyombo vya habari wamekuwa wakiwahoji mashabiki wa
Yanga ambao wanazungumza kama viongozi.
0 COMMENTS:
Post a Comment