UHUSU (WA PILI KUSHOTO) AKIWA NA WACHEZAJI WENGINE WA ROYAL EAGLES. |
Mshambuliaji wa Royal Eagles, Uhuru Selemani amesema anataka
kufanya vizuri zaidi ili apate nafasi katika kikosi cha Taifa Stars.
Uhuru aliyewahi kuzichezea Simba na Mtibwa Sugar, amesema bado anataka kuwa kati ya wachezaji wanaolisaidia
taifa.
“Nakumbuka kipindi kile niko kwenye kikosi cha Taifa Stars ya
Marcio Maximo. Utaifa ni kitu kikubwa sana kwa mtu ambaye anataka mafanikio ya
nchi yake.
“Bado natamani kuwa miongoni mwa wale wanaotoa msaada kwa taifa
langu.
“Lakini ninajua ili nipate nafasi hiyo, lazima nizidi kujituma na
kufanya vizuri katika kikosi cha timu yangu hapa,” alisema.
Tayari Uhuru amefunga mabao mawili katika mechi zake mbili za Ligi
Daraja Afrika Kusini akiitumikia Royal Eagles ya jijini Darbun.
0 COMMENTS:
Post a Comment