AMINA. |
Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake
nchini (TWFA), Amina Karuma anatarajiwa kuhudhuria kuhudhuria kongamano la
viongozi wa soka la wanawake duniania litakalofanyika Zurich nchini Uswisi
Septemba 28 – 02 Oktoba, 2015.
Kongamano hilo linashirkisha viongozi 35 wanawake wa
mpira wa miguu kutoka semehu mbalimbali duniani ikiwa ni muendelezo wa
kongamano liliofanyika mwezi Machi mwaka huu Vancouver Canada wakati wa fainali
za kombe la Dunia la Wanawake.
Programu hiyo ya viongozi wa wanawake ni sehemu ya
mikakati ya FIFA ya kuongeza idadi ya viongozi wengi wa soka wanawake duniani
katika utawala wa mpira wa miguu wa wanawake.
0 COMMENTS:
Post a Comment