Ndiyo mpira ulivyo, usishangae
kuona Barcelona akipokea kipigo cha paka mwizi katika La Liga ambayo huonyeshwa moja kwa moja na Azam TV.
Celta Vigo imeitwanga Barcelona kwa
mabao 4-1 katika mechi ya Ligi Kuu Hispania maarufu kama La Liga.
Nolito na Iago Aspas walikuwa
mashujaa baada ya kupachika mabao mawili mapema ana kuifanya timu yao kwenda
mapumziko ikiwa inaongoza.
Pamoja na juhudi za dhati za
Barcelona katika kipindi cha pili ikiwatumia Neymar, Messi na Suarez lakini
bado mambo hayakuwa walivyotaka kabla ya Bilbao kuongeza bao la tatu.
Neymar aliifungia Barcelona bao
ikionekana kama watapambana na kusawazisha lakini Celta Vigo wakaongeza bao la
nne.
Beki Gerard Pique alionekana kuwa
katika kiwango cha chini kwa kuchangia mabao mawili kutokana na kutokuwa
makini.
0 COMMENTS:
Post a Comment