September 16, 2015

MPIRA UMEKWISHAAAAAAA
Dk 90+2
Dk 90, Busungu anapiga shuti kali lakini linapita juu kidogo

Dk 86, Niyonzima anapoteza nafasi nyingine ya kufunga bao



SUB Dk 85, anatoka Tambwe anaingia Malimi Busungu

Dk 74 81, Yanga wanaonekana kulishambulia zaidi lango la Prisons lakini wanapoteza nafasi nyingi za kufunga
Dk 71 Tambwe anapiga shuti kali akiunganisha krosi ya Niyonzima lakini kipa anaokoa na kuwa kona

Dk 67, Telela anapiga shuti kali baada ya krosi nzuri ya Msuva, lakini unaokolewa

SUB Dk  66, Yanga inamuingiza Salum Telela badala Kaseke

Dk 59 Krosi nzuri ya Niyonzima inamkuta Tambwe lakini anashindwa kufanya lolote

GOOOOOOO Dk 60 Ngoma ANAFUNGA VIZURI KWA SHUTI KALI.


Dk 59 Yanga inapewa penalti kutokana na adhabu hiyo
KADI NYEKUNDU DK 59 James Josephat analambwa kadi nyekundu baada ya kumuangusha Msuva.
Dk 58, mpiara mzuri wa adhabu wa Niyonzoma, unatua kichwani kwa Tambwe lakini anashindwa kulenga akiwa yeye na kipa.

Dk 51, Prisons wanaonekana kukichafua, zaidi wanacheza kibabe hali inayomlazimu Kocha Pluijm kuanza kulaumu.


Dk 47, kimenya anapiga shuti kali lakini Barthez anafanya kazi ya ziada na kuokoa. Inakuwa kona lakini haina matunda kwa Prisons.
MAPUMZIKO
GOOOO Dk 45, Tambwe anaipatia Yanga bao la pili
Dk 41, Yanga wanaonekana kucharuka na kufanya mashambulizi mengi zaidi
Dk 35, Tanga anapata mpira mzuri ndani ya eneo la hatari lakini anashindwa kugeuka haraka

Dk 32, bado Prisons hawajapiga hata shuti moja lililolenga lango la Yanga. 
GOOOO Dk 27, Yanga wanapata bao baada ya Twitte kupiga shuti kali kutokana na piga nikupige kwenye lango la Prisons.

 Dakika ya 23 sasa, inaonekana habari ni ileile, hakuna shambulizi kubwa wala shuti hata moja langoni. Timu zaidi zinacheza katika ya uwanja.

Dk 16 sasa, lakini mpira zaidi unachezwa katikati na hakuna hata timu moja katika dakika zote 5 iliyofanya shambulizi hata moja.

Dk 11, Msuva anaingia vizuri baada ya pasi nzuri ya Niyonzima, lakini Prisons wanaokoa na kuwa kona isiyokuwa na matunda.

Mechi imeanza Yanga, imeanza kwa kasi na Yanga ndiyo wanaojaribu kufika kwenye lango la Prisons mfululizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic