Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa
kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa kwa siku za jumamosi na
jumapili katika viwanja nane tofauti nchini ikiwa ni mzunguko wa tatu tangu
kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika mechi hizo, Azam TV pekee ndiyo itakayoonyesha moja kwa moja na kuwapa nafasi wapenda soka wasio uwanjani au katika mikoa mechi zinazochezwa kushuhudia mzigo huo saaafi.
Jumamosi mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya
Young Africans watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam, Chama la Wana Stand United watawakaribisha Wana Kimanumanu African
Sports katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga.
Jijini Mbeya kutakua na mpambano wa wenyeji wa mji huo
(Mbeya Derby) kati ya Tanzania Prisons watakapokuwa wakipambana na Mbeya City
katika uwanja wa Sokoine jijini humo, huku Maafande wa Mgambo Shooting
wakiwakaribisha Wana Lizombe Majimaji FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa michezo minne
kuchezaw, Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam, huku Mwadui FC wakiwa wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Mwadui
Complex mjini Shinyanga.
Wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha
Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na Wagosi wa Kaya
Coastal Union watakua wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga
0 COMMENTS:
Post a Comment