Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi kesho Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja
mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza kusaka
nafasi tatu za juu ili kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Kundi B, Polisi Morogoro watacheza na Burkina Faso
uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji FC watacheza na Kurugenzi uwanja wa
Amani mjini Njombe, Lipuli ya Iringa watawaribisha Kimondo FC uwanja wa Wambi-
Iringa na JKT Mlale watakua wenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Majimaji
mkoani Ruvuma.
Kundi C, Mbao FC watawakaribisha Geita Gold uwanja wa
CCM Kirumba, Rhino Rangers watacheza dhidi ya Polisi Tabora uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja
wa Ushirka mjini Moshi na Polisi Mara watakua wenyeji wa JKT Kanembwa kwenye
uwanja wa Karume mkoani Mara.
0 COMMENTS:
Post a Comment