MAJABVI |
Kiungo wa Simba, Justice Majabvi, raia wa
Zimbabwe, amewaambia mashabiki wa soka hasa wa timu yake kuwa hawatakiwi
kuukosa mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Yanga, kwani atahakikisha kiungo wa
Yanga, Thabani Kamusoko hatambi katika eneo hilo.
Majabvi na Kamusoko wote ni raia wa Zimbabwe
ambapo kwa michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara ambayo wote kwa pamoja wamefanikiwa
kucheza mpaka sasa, mashabiki wa Simba na Yanga wameonekana kuvutiwa nao huku
kila upande ukisema kiungo wao ndiye bora.
Ili kuondoa utata huo, Majabvi amesema , mashabiki hawapaswi kuwafananisha kihivyo, bali wanatakiwa
kutoikosa mechi hiyo na kuangalia jinsi wanavyoonyeshana kazi.
“Najua tuna mchezo mkubwa wikiendi hii huku pia
mashabiki wakitaka kuondoa utata wa mimi na Kamusoko nani zaidi, binafsi siwezi
kusema lolote zaidi ya wao wenyewe kuja kuona itakavyokuwa.
“Kwa upande wangu nimejipanga na hilo na namjua
Kamusoko vizuri, hivyo basi nina uhakika nitamshinda na kuishinda timu yake
pia, kwa maandalizi tuliyoyafanya tunatarajia kupata ushindi wa aina yoyote ule
na siwezi kutoa ahadi kwamba lazima tuwafunge mabao fulani kwani ushindi ni
ushindi tu, muhimu ni pointi tatu,” alisema Majabvi.
0 COMMENTS:
Post a Comment