Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema anataka kikosi chake
kuendeleza ushindi kwenye Ligi Kuu Bara bila ya kujali kinakutana na nani.
Azam FC itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, Jumapili.
Hall amesema anatambua ubora wa Mbeya City na kuwa ni moja ya timu
zilizojiandaa vema, yenye tamaa ya mafanikio.
“Yote hayo ninayajua, lakini ninapenda kuhakikisha tunashinda kila
mechi iliyo mbele yetu,” alisema.
“Maandalizi yanaendelea, kila mchezo mbele yetu tunaupa ukubwa au
uzito wa namna yake.”
Mbeya City imekuwa ina mwendo wa kusuasua ingawa tokea kuanza kwa
msimu huu ingawa inaisumbua sana Azam FC kila inapokutana nayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment