Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa makampuni ya Quality group, Yusuf Manji
ameibuka mshindi wa tuzo maarufu ya Mfanyabiashara Gwiji Duniani.
Manji ambaye ni mwenyekiti wa mabingwa wa soka
Tanzania Bara, Yanga ameibuka mshindi wa tuzo hiyo na kuwashinda mabosi wengine
kama bilionea namba moja Afrika Aliko Dangote.
Kwa mujibu wa mtandao wa Business Forum, Mwenyekiti
huyo wa amekuwa kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kushinda tuzo hiyo ambayo
awali walikuwa wakichukua matajiri wengine wakubwa na maarufu kutoka katika
mabara ya Amerika, Ulaya na Asia.
Msemaji wa Quality Group, Smitha Swamy jana
alithibitisha Manji kushinda tuzo hiyo, lakini akasema atakuwa tayari
kulizungumzia hilo, leo.
“Ni kweli, lakini leo nimebanwa. Nitalizungumzia hilo
kesho,” alisema.
Baadhi ya waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni Mwenyekiti wa
Emirates Group, Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum inayomiliki kampuni ya Ndege
ya Emirates inayozidhamini timu za Real Madrid, Arsenal, AC Milan na nyingine
kubwa.
Wengine ni Mwenyekiti wa Emmar
Properties, Mohammed Alabbar pia bilionea kutoka India, Ratan Tata
anayemiliki kampuni kubwa ya Emeritus of Tata Sons Ltd.
Pia bilionea aliye tano bora duniani kwa utajiri,
Mukesh Ambani ambaye ni mwenyekiti wa Reliance Industries Ltd. Wengine ni
Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand.
Pamoja na ushindi huo wa kishindo wa Manji dhidi ya
matajiri wengine wakubwa Afrika na duniani kote, Kampuni yake ya Quality
Group imeshinda kuwa kampuni bora na yenye mpangilio wa uhakika kwa bara la
Afrika ikipewa tuzo ya “Most Iconic Brand 2015”.
0 COMMENTS:
Post a Comment