BUSUNGU AKIWA KATIKA BENCHI LA YANGA, JANA. |
Straika
mpya wa Yanga, Malimi Busungu ataendelea kupambana hadi siku atakapopata nafasi
ya kudumu.
Busungu
amesema anajiamini, lakini anaamini uwezo wa wanaopata nafasi katika kikosi cha
Yanga kwa sasa.
“Kweli
kuna wachezaji wazuri pia ninalazimika kupambana kweli kupata namba. Lakini
ninaamini nitaweza, ni suala la muda tu.
“Nataka
kuitumia vizuri kila nafasi ninayopewa na mwalimu. Iko siku utaona tu,”
alisema.
Mara
nyingi, Busungu ambaye amejiunga na Yanga akitokea Mgambo Shooting amekuwa
akiingia kipindi cha pili.
Wakati Kocha Hans van der Pluijm anaonekana kuwaamini zaidi washambuliaji wageni, Donald Ngoma kutoka Zimbabwe na Mrundi, Amissi Tambwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment