BRAHIMI AKIPAMBANA NA OZIL NA KHEDIRA WA UJERUMANI |
Beki kisiki wa Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
amekiri kukumbwa na ugumu wa kumkaba mshambuliaji wa Algeria, Yacine Brahimi,
anayekipiga na timu ya FC Porto ya Ureno.
Stars
na Algeria zinakutana Novemba 14 huku mechi ya marudiano ikichezwa Novemba 17
katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa
kufanyika Urusi mwaka 2018.
Algeria
ndiyo timu bora Afrika kwa mujibu wa viwango vya Fifa na ndiyo timu iliyofanya
vizuri zaidi kwenye Kombe la Dunia mwaka jana kwa upande wa timu za Afrika.
Cannavaro
amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwa upande wao kutokana na wachezaji wa timu
hiyo kucheza soka la kulipwa Ulaya na kudai kuwa uwezo wa Yacine Brahimi ambaye
ndiye anatarajia kumkaba ni mkubwa, hivyo anahitaji umakini wa hali ya juu.
“Inabidi
tuombe Mungu atusaidie, Algeria ni timu namba moja Afrika, hivyo tunatarajia
kukutana na ugumu wa hali ya juu, hasa ukizingatia wachezaji wao wengi
wanacheza soka la kulipwa Ulaya.
“Brahimi
ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa, hivyo nitakuwa na kibarua kigumu kuweza
kukabiliana naye kutokana na uwezo alionao,” alisema Cannavaro.
0 COMMENTS:
Post a Comment