Mshambuliaji nyota wa Simba, Hamis Kiiza atakuwa nje ya
uwanja kwa wiki mbili akiuguza maumivu ya nyama za paja akiwa mazoezini.
Kiiza raia wa Uganda aliyejiunga na Simab msimu
huu akitokea Yanga ambaye sasa anaongoza kwa ufungaji katika Ligi Kuu Bara
akiwa na mabao matano, alipata maumivu hayo mazoezini Jumanne iliyopita.
Wakati Mganda huyo akikaa nje ya uwanja kwa
wiki mbili, kiungo mchezeshaji Mwinyi Kazimoto yeye amerejea uwanjani na kuanza
mazoezi mepesi akitoka katika majeruhi ya enka.
Daktari wa
Simba, Yassin Gembe, alisema uamuzi huo wa kumuweka Kiiza nje ya uwanja umekuja
baada ya kumfanyia vipimo vya majeraha hayo.
Gembe alisema ndani ya wiki hizo mbili, Kiiza
ataitumia wiki moja kwa kupewa matibabu na wiki nyingine ataitumia kwa kufanza
mazoezi mepesi ya binafsi kabla ya kujiunga na wenzake.
Hii inamaanisha kuwa, huwezekano wa Kiiza
kucheza au kutocheza mechi dhidi ya Mbeya City Oktoba 17, mwaka huu kwenye
Uwanja wa Sokoine, Mbeya itategemea na maendeleo ya afya yake.
“Kiiza tumemfanyia vipimo leo (jana) mchana na
amegundulika ana maumivu makali ya nyama za paja yatakayomuweka nje ya uwanja
kwa kipindi cha wiki mbili.
“Katika kipindi hicho chote atafanya program
maalum aliyopewa na madaktari waliomfanyia vipimo ikiwemo kupata matibabu kwa
wiki ya kwanza kabla ya pili kuanza mazoezi mepesi ya binafsi,” alisema Gembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment