Staa wa zamani wa Simba, Uhuru Suleiman sasa
anakipiga katika Klabu ya Royal Eagles ya Afrika Kusini kwa mkopo akitarajiwa
kurejea Jomo Cosmos, lakini Mamelodi Sundowns nayo inamtaka.
Awali Jomo Cosmos ndiyo iliyomsajili baada ya
Simba ‘kumkaushia’ lakini alipofika Afrika Kusini, klabu hiyo ya Ligi Kuu
Afrika Kusini ikampeleka kwa mkopo Royal Eagles ya Daraja la Kwanza ili
aboreshe kiwango chake.
Kwa mujibu wa Uhuru mwenyewe, sasa yupo vizuri
na akiwa katika harakati za kurejea Jomo Cosmos, taarifa zimemfikia kuwa Mamelodi
wanataka kumsajili.
“Januari mwakani natakiwa kurejea Jomo Cosmos,
lakini wakala wangu ameniambia amefuatwa na watu kutoka Mamelodi wakitaka
kunisajili bada ya kuvutiwa na uwezo wangu,” alisema Uhuru.
“Nafurahi kuona mambo yanaenda hivi, lakini
hatma ya wapi nitacheza itafahamika Januari kwani ni lazima tufikie makubaliano
mazuri.”
0 COMMENTS:
Post a Comment