MAJABVI |
Simba imeambiwa wala isiwe na papara kikifika
kipindi cha usajili wa dirisha dogo kwani ikitaka italetewa straika hatari
zaidi ya Donald Ngoma wa Yanga ambaye ana mabao manne katika Ligi Kuu Bara.
Aliyetamka maneno hayo ni kiungo Justice
Majabvi wa Simba, ambaye ameona timu yake haina mastraika wengi uwanjani, hivyo
waliopo wakiumia tu hali huwa si nzuri.
Majabvi alisema: “Kama Simba ikitaka kusajili
tena, nadhani utakuwa wakati wa kutazama vipaji kutoka kwetu Zimbabwe ambako
kuna wachezaji wengi wazuri.”
“Wachezaji hao wengi ni wa gharama nafuu, kuna
washambuliaji wakali kuliko yule Ngoma anayeonekana anajua sana Yanga, kama
viongozi wakihitaji nipo tayari kutafuta straika mkali na wachezaji wengine.”
Majabvi alisema Zimbabwe inaaminiwa kuwa na
wachezaji wengi wenye vipaji, ndiyo maana wamejaa katika Ligi Kuu Afrika Kusini
wakicheza soka la kulipwa.
Simba ina mastraika wanne ambao ni Hamisi
Kiiza, Mussa Mgosi, Ibrahim Ajibu, Boniface Maganga na Pape N’daw.
0 COMMENTS:
Post a Comment