Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Free State Stars ya
Afrika Kusini, Mtanzania, Mrisho Ngassa, juzi Jumamosi aliisaidia timu yake kutinga
hatua ya robo fainali ya Kombe la Telkom Knockout, baada ya kuichapa Bidvest
Wits bao 1-0.
Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Goble
Park jijini Bethlehem, Ngassa alifanikiwa kucheza kwa dakika zote 90.
Bao pekee la timu yao lilifungwa na kiungo wa timu
hiyo, Danny Venter katika dakika ya 72 ya mchezo huo.
Ngassa alikuwa akihaha uwanja mzima na kuwapa wakati mgumu wapinzani wao huku akiwachosha mabeki waliokuwa wakitumia nguvu sana.
Baada ya mchezo huo, jana Jumapili Ngassa
alitarajiwa kutua nchini kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars
ambacho kinajiandaa na mchezo wa kusaka nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia ambapo
keshokutwa Jumatano kinatarajiwa kucheza dhidi ya Malawi kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar.
Ikumbukwe kuwa, uongozi wa Free State uliomba kiungo
huyo achelewe kujiunga na kambi ya Stars iliyoanza Oktoba Mosi ili tu aweze
kucheza mchezo huo ambao ulikuwa muhimu kwao.
0 COMMENTS:
Post a Comment