Na Saleh Ally
Suala la beki
wa Mbeya City, Juma Nyosso limechukua sura mpya baada ya kuzua mjadala barani
Ulaya.
Pamoja na
kujadiliwa mitandaoni, gazeti la siasa la Sweden la Aftonblandet limeandika
katika ukurasa wake wa michezo likimjadili Nyosso ambaye amefungiwa kucheza
miaka miwili na kulipa faini ya Sh milioni 2 baada ya kumdhalilisha nahodha wa
Azam FC, John Bocco kwa kumtomasa makalio, wiki iliyopita.
Gazeti hilo
kupitia ukurasa wake Sportsbladet limelielezea suala hilo la Nyosso kuwa ni
sehemu ya mambo ya kushangaza katika soka kwa sababu mbili.
Katika ukurasa
huo wa michezo, gazeti hilo lililotoka wiki iliyopita lenye kichwa cha habari “Stangs av I tva
ar-for oanstandigt uppforande” yaani afungiwa kucheza soka kwa tabia chafu,
lilijichanganya kumuita Nyosso ni beki tegemeo wa Taifa Stars tena likitumia
picha akiwa na jezi ya Taifa Stars wakati akiichezea.
Hata hivyo,
mjadala wa gazeti hilo ulikuwa ni adhabu ya Nyosso kuonekana ni kubwa sana huku
baadhi ya waliojadili wakisisitiza, angefungiwa mechi kadhaa.
Wengine kama
ilivyo kwa wadau wa soka nchini, walieleza kwamba Nyosso alistahili kupata
adhabu kali kwa kuwa alirudia kufanya tendo hilo, lakini si kufungiwa muda
mrefu hivyo.
Suala hilo,
limekuwa mjadala hata hapa nchini wengine wakiunga mkono adhabu hiyo ya TFF na
wengine wakitaka ipunguzwe, wengine wakisisitiza itumike moja iwe kufungiwa au
faini na si zote kwa wakati mmoja.
Kabla ya
kumfanyia hivyo Bocco kwa mkono wake wa kushoto, Nyosso aliwahi kufanya hivyo
kwa mkono wake wa kushoto kwa Elius Maguli akiwa Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment