Na Saleh Ally
Leo ndiyo
kile kipute kati ya Tanzania dhidi ya Malawi kuwania kucheza Kombe la Dunia.
Mechi hiyo inachezwa leo kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam na inaonekana mashabiki wengi wana matumaini makubwa.
Ukubwa wa matumaini unafanya mechi hiyo
ionekane kama ni lahisi jambo ambalo si sahihi.
Huenda wako wanaamini ni lahisi kwa kuwa
Tanzania ilitoka sare na Nigeria ambao ni ulinganisho usio sahihi.
Lazima wachezaji Stars wacheze wakiamini
mchezo ni mgumu na wanatakiwa kushinda leo ili kujiwekea mazingira bora hapo
baadaye.
Malawi wana wachezaji nane wanaocheza nje ya
nchi yao. Ni nchi za jirani za Msumbiji na Afrika Kusini ambazo zimepiga hatua
kisoka zaidi yao.
Lakini wana timu ya wachezaji vijana zaidi. Hivyo
lazima tukubali wana timu nzuri na yenye ushindani mkiubwa.
Ukichana na hivyo, wamekutana na Tanzania mara
nne, wameshinda mara mbili, sare moja na tumewafunga mara moja. Lazima tukubali
mechi ya leo ni ngumu.
0 COMMENTS:
Post a Comment