October 7, 2015


Sasa ni mapumziko, Tanzania au Taifa Stars inaongoza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Samatta ndiye alianza kufunga kwa pasi nzuri ya Ulimwengu ambaye alifunga bao la pili baada ya kipa wa Malawi kutema mkwaju wa krosi wa Haji Mwinyi na Ulimwengu akafanya kuusukumizia mpira wavuni.

Mechi ilikuwa ni ngumu kwa kila upande, Malawi ndiyo waliopeleka mashambulizi mengi zaidi ya Taifa Stars hasa kataika dakika 15 za mwanzo.


Lakini kuanzia dakika 20 hadi 35, Stars walionekana kuutawala mpira zaidi lakini bado Malawi hawakuwa wamelala.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic