October 31, 2015



MPIRA UMEKWISHAAAAA
SUB Dk 90, Ngoma anakwenda nje nafasi yake anachukua Matheo Simon

Dk 90, Kulachi anapiga shuti kali, Dida anaokoa unamkuta Ngwai naye anapiga shuti linatka nje

SUB Dk 86, Kaseke anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya


Dk 80 hadi 84, Yanga wanaonekana kuumiliki mpira zaidi lakini kwa lengo la kuhakikisha KAgera hawaupati na kuwashambulia
 KADI Dk 79 Idi Kulachi wa Kagera analambwa kadi ya njano kwa kumkanyaga kwa makusudi Haji Mwinyi

KADI Dk 78, mwamuzi anampa Ngoma kadi ya njano kwa kupoteza muda

Dk 76, Msuva anapata mpira nje ya eneo la 18, anapiga shuti kali lakini kipa Agathon anadaka kwa ustadi mkubwa

Dk 70, Ngoma anashindwa kuifungia Yanga baada ya kumpiga chenga beki, anabaki yeye na kipa lakini anashindwa kufunga

Dk 65 hadi 69, Kagera ndiyo wanaonekana kutawala mpira lakini wanahsindwa kufunga
Dk 64, Iddi Kulachi anapiga krosi safi, kabla haijamfikia Mgwai Yondani anaondosha

Dk 64, Kanoni anapiga shuti kali, Dida anatema lakini Yondani anawahi na kuondosha
GOOOOOOO Dk 62, Kaseke anaindikia Yanga bao la pili baada ya Tambwe kupiga shuti, likaokolewa na kipa lakini Kaseke akauwahi na kufunga bao lake la kwanza la ligi akiwa na Yanga

DK 60, Tambwe anapiga shuti kali sana lakini Job anatandika reli mpira unatoka na kuwa wa kurushwa

Dk 59, James Josephat anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Ngoma lililokuwa limelenga lango
Dk 56 Niyonzima anachonga kona safi, Ngoma anaruka na kupiga kichwa lakini inakuwa ni goal kick

SUB Dk 53, Yanga inafanya mabadiliko ya kwanza kwa kumtoa Busungu na nafasi yake inachukuliwa na Simon Happygod Msuva

dk 51, Masumbuko tena anapata nafasi ya kuisawazishia Kagera baada ya pasi nzuri ya Kavila, lakini anashindwa tena kupiga shuti vizuri

Dk 49, Masumbuko anapata nafasi nzuri lakini anapiga shuti dhaifu linalodakwa na Dida kwa ulaini

Dk 46, Kagera wameanza kwa kasi wakionekana kuwa wamepania kuhakikisha wanashinda. Hata hivyo kila wanapokaribia lango mashambulizi yao yanakuwa si makali ya kutisha


MPIRA MAPUMZIKOOO
Dk 45, Ngwai akiwa nje ya 18 ya Yanga anapiga shuti kali lakini kipa Dida anadaka kwa ulaini kabisa

Dk 43 hadi 44, mpira unaonekana hauna radha sana kwa kuwa kila upande unahofu na ubora wa uwanja hivyo kubutua kunachukua nafasi kubwa zaidi

Dk 42 mwamuzi anamuonya kwa mdomo tu Kanoni ambaye anamrukia Kaseke ambaye sasa anatibiwa

Dk 40, krosi nyingine nzuri ya Kagera, Bossou anauwahi na kuutoa nje, kona inayochongwa na Kanoni lakini Yondani anapiga kichwa na Ngoma anaondosha kabisa hatari hiyo.

Dk 39, Yanga wanapata kona, inachongwa na Niyonzima, mabeki wa Kagera wanawahi kuondosha


Dk 39, Kavila anapiga krosi nyingine safi lakini Yondani anawahi kuondosha eneo la hatari

KADI Dk 38, Haji Mwinyi analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Kanoni wa Kagera

Dk 36, Kaseke anafanikiwa kumtoka kipa Agathony na kupiga krosi lakini mabeki wa Kagera wnaawahi na kuokoa.

Dk 29 hadi 32, mpira unachezwa zaidi katikati huku kila timu ikiosha zaidi hali inayoonyesha kutokana na kila upande kuhofia kufanya makosa kutokana na hali ya uwanja


Dk 28, Ngoma anawatoka mabeki wawili wa Kagera, anatoa pasi nzuri ya nyuma kwa Tambwe lakini hata hivyo anapiga krosi laini

Dk 25, Mtiro anapiga mpira mzuri wa krosi katika lango la Yanga lakini wenzake wa Kagera wanacheza faulo. Abdul Jaffar anamsukuma Yondani

GOOOOOO Dk 23, Ngoma anafunga bao safi kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Juma Abdul Jaffar kutoka kulia mwa uwanja

Dk 20, Tambwe anaingia vizuri katika eneo la hatari lakini Ibrahim Job anaokoa vizuri


Dk 15, hatari katika lango la Kagera baada ya George Kavila kurudisha mpira mfupi, Ngoma anauwahi lakini anashindwa kumalizia


DK 9 hadi 12, uwanja nao unaonekana kuwa kikwazo kwa kila upande 

Kila upande unaonekana kushambulia  kwa zamu ingawa karibu mashambulizi yote yanaishia katikati ya uwanja.


Hadi sasa hakuna shambulizi kali lililotikiza upande mwingine.

1. Deo Munish-30
2. Juma Abdull-12
3. Mwinyi Hajji-20
4. Yondani Kelvin-5
5. Vicent Bossou-9
6. Twitte Mbuyu-6
7. Busungu Malimi-16
8. Haruna Niyonzima -8
9. Tambwe Amiss-17
10. Donald Ngoma
11.Deus Kaseke-4
SUB
GK. Alli Mustapha-1
2. Pato Ngonyani-15
3. Nadir Haroub-23
4. Simon Msuva-27
5. Matheo Anthony-10
6. Saidi Juma-22
7. Geofrey Mwashiuya-19
COACH.
Hans Van Der Pluijm


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic