October 21, 2015


MPIRA UMEKWISHAAAAAA
KADI NYEKUNDU Dk 90+2 Hassan Hatibu, analambwa kadi ya pili ya njano, inakuwa nyekundu na anakwenda njeDk 90+5
GOOOOOOOOOO Dk 90 Msuva anafunga bao safi sana kwa kuunganisha krosi nzuri ya Coutinho

 Dk 89, Sheva Go anawatoka Cannavaro na Bossou lakini wanaokoa na kuwa kona isiyokuwa na matunda

Dk 88, Ngoma anapewa pasi nzuri, akiwa katika nafasi nzuri anapiga shuti la chini lakini kipa anaokoa kw amiguu

Dk 84, Busungu anapiga krosi nyingi safi inamfikia Tambwe anapiga kichwa lakini ni goal kick

GOOOOOOOOO Dk 81, Tambwe anafunga bao safi baada ya Busungu kugongeana na Msuva kabla ya kupiga krosi saafi iliyotua katika mguu wa Tambwe ambaye anafikisha bao la tano sawa na Ngoma na Hamisi Kiiza

Dk 77 krosi nyingine safi ya Coutinho inaingia ndani, Toto wanaokoa na kuwa kona, inachongwa lakini haina madhara

DK 74, Coutinho anapiga mpira safi wa adhabu lakini Bossou akiwa na lango pekee anashindwa kufunga

SUB Dk 69, Yanga wanamtoa YOndani aliyeumia, nafasi yake inachukuliwa na Nadir Haroub 'Cannavaro'

SUB DK 67 Mwashiuya anatoka, nafasi yake inachukuliwa na Coutinho ambaye hii ndiyo mechi yake ya kwanza

Dk 66, Sheva Go tena, nje ya eneo la 18 la Yanga anapiga shuti lakini Barthez anajituma na kudaka vizuri
KADI Dk 65, Tambwe anashindwa kuiwahi krosi na kulazimika kuushika mpira, mwamuzi anampa kadi ya njano kwa uzembe

Dk 64 krosi nzuri ya Msuva inakwenda kichwani kwa Tambwe lakini anaashindwa kulenga lango, goal kich

Dk 62, Ttoto African wanafanya shambulizi jingine, Sheva Go anajitahidi kuuwahi mpira lakini anachelewa na Yondani anaokoa 
Dk 61, Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira safi wa krosi unaogonga kwenye kona ya mtambaa wa panya

Dk 56, Sheva Go, anaingia katika eneo la 18 la Yanga na kupiga shuti zuri, BArthez anadaka na kutema lakini anauwahi tena


GOOOOOOOO Dk 55, Madenge au Sheva Go anaifungoa Toto bao kwa kichwa ambalo ni la tatu kwake msimu huu. Alifunga baada ya krosi kali ya Seseme iliyookolewa na BArthez na kumkuta yeye aliyemzidi ujanja Yondani na kufunga
Dk 53, Tambwe anaingia ndani katika eneo la hatari, anajaribu kumpa Ngoma krosi lakini hesabu zake zinakuwa mbovu na kipa wa Toto anadaka.


GOOOOOO Dk 48 Msuva anaingia ndani ya eneo la hatari la Toto na kufunga bao safi kabisa


Dk 46, Msuva anaingia katika eneo la hatari na kupiga shuti kali lakini anashindwa kufunga

Dk 46 Yanga inamuingiza Msuva MAPUMZIKO
DK 45+2 Tambwe anapoteza nafasi nyingine tena akiwa katika nafasi nzuri 
DK 45+1 Ngoma anapiga mpira wa penalt na kukosa.....PENAAAAAAT Dk 45, mwamuzi anatoa penalt baada ya Carlos Protas kushika mpira wakati akiokoa krosi ya Ngoma
Dk 41, Niyonzima anaingia vizuri na kupiga krosi nzuri, inamkuta Kamusoko ambaye anapiga shuti kali lakini linatoka nje

KADI Dk 37, nahodha wa Toto HAssan Hatibu analambwa kadi ya njano kwa kufanya faulo ya kijinga kwa kumuangusha MWahiuya

Dk 34, Ngoma anapata nafasi zaidi anapiga shuti kali lakini linapita juu ya lango

Dk 28, Toto wanafanya shambulizi kali, lakini Bossou anaweza kuookoa mpira kwa kupiga kichwa

Dk 16 hadi 22, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja huku Toto wakiwa hawajafanya shambulizi jingine tena Dk 14, Toto wanafanya shambulizi kubwa la kwanza na kupata kona, inapigwa na Miraji Madenge 'Sheva Go' anapiga shuti kali lakini linapita juu

Dk 13, Tambwe akiwa ndani ya eneo la hatari la Toto anageuka na kupiga shuti kali, lakini linatoka kidogo
GOOOOOOOO Dk 9, Juma Abdul anapiga shuti kali sana na kuiandikia Yanga bao.

Dk 8 Ngoma anaingia vizuri, anapiga shuti kali lakini kipa anaokoa na kuwa kona
Dk 6, BArthez anafanya kosa kwa kurusha mpira haraka, mpira anauwahi Japhet Makaranga 'Balotelli', hata hivyo naye anashindwa kufunga
Dk 5, Kamusoko anapiga mpira wa adhabu vizuri kabisa lakini mpira unatka na ku[piga nyavu za nje

DK 4, nafasi nyingine kwa Tambwe, Mwashiuya alipiga shuti kali likambabatiza yeye Tambwe, lakini akashindwa kufunga baada ya kuuwahi mpira

Dk 1, Yanga wanakuwa wa kwanza kufika langoni mwa Toto na kufanya shambulizi linalozaa kona, inapigwa na mpira unamkuta Tambwe akiwa na kipa, alakini anashindwa kufunga

Hivi punde tutawaletea moja kwa moja mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Toto African.



Timu hizo ambazo hujulikana kama ndugu zinakutana kuwania pointi tatu kila upande, Yanga ikiwa kileleni na pointi 16 na Toto African wakiwa na 10 katika nafasi ya 10.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic