Cristiano Ronaldo
ameonyesha mapenzi ya juu kwa shabiki aliyevamia uwanjani.
Shabiki huyo alivamia
uwanjani wakati Madrid ikipambana na PSG iliyokuwa nyumbani jijini Paris,
Ufaransa.
Ilikuwa ni mechi ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya, shabiki huyo alikatiza kwa kasi ya kimondo. Alipomfikia Ronaldo,
alimpokea na kumkumbatia.
Hata wakati walinzi wa
uwanja wanaingia, Ronaldo aliwazuia kumpa kipigo, akapiga naye stori sekunde
kadhaa na kuwaruhusu wamchukue lakini si kwa kumpiga.
Baada ya hapo mashabiki
walimshangilia kwa kile alichoonyesha kwa shabiki huyo aliyeonyesha mapenzi
makubwa kwake.
0 COMMENTS:
Post a Comment