Maisha ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho,
ndani ya kikosi hicho kwa sasa yanaweza kuwa mafupi kufuatia uongozi wa klabu
hiyo kumuweka katika hesabu za kumpiga bei endapo watapata ofa nzuri kutoka kwa
timu yoyote ile.
Coutinho ambaye aliletwa nchini na aliyekuwa kocha wa timu hiyo,
Mbrazili, Marcio Maximo, kwa sasa hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu
hiyo ambapo mara kwa mara kiungo huyo amekuwa akiomba kuuzwa ili kulikwepa
benchi.
Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alisema klabu hiyo ipo tayari
kumuuuza Mbrazili huyo ambaye alipoingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo
dhidi ya Toto wiki iliyopita, alionyesha kiwango kikubwa, akiwa anacheza kwenye
ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu.
“Tupo tayari kumuuza Coutinho
iwapo itatokea dau lolote kubwa na tutamuacha aende, lakini hatuna mpango wa
kumuacha kwenye dirisha dogo, tupo tayari kumuuza mchezaji yeyote yule kwa
kuangalia dau kubwa.
“Lakini tutafanya hivyo endapo kama itatokea timu yoyote ile
ambayo itakuwa tayari kukubaliana na sisi juu ya bei ya kumuuza kiungo huyo na
tukishaafikiana, hatutakuwa na sababu ya kumzuia kuendelea kuwepo ndani ya
kikosi chetu,” alisema Tiboroha ambaye ni mhadhri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
0 COMMENTS:
Post a Comment