MAGULI (KUSHOTO) PAMOJA NA HARUNA CHANONGO WAKISHANGILIA BAO ALILOFUNGA STRAIKA HUYO WA ZAMANI WA SIMBA... |
Baada ya straika wa Stand United, Elias
Maguli kufanikiwa kufikisha mabao nane na kuwa kinara kwenye ligi kuu,
aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Simba na sasa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe,
amefunguka kuwa ni vizuri amewaumbua na wajue walichokifanya hakikuwa sahihi.
Maguli aliachawa na Simba kama ilivyokuwa kwa
Tambwe kwa madai viwango vya washambuliaji hao havikuwa vizuri na timu
walizotimkia wamekuwa gumzo kutokana na kuwa na viwango bora za ufumaniaji wa
nyavu.
Maguli mpaka sasa katika michezo nane,
amefunga mabao nane huku Tambwe akiifungia Yanga mabao matano katika michezo
saba. Msimu uliopita Mrundi huyo alifunga mabao 14 akiwa wa pili huku msimu wa
2013/14 akifunga mabao 19.
Straika huyo Mrundi amesema anampongeza Maguli kutokana na uwezo wake wa kuzifumania nyavu
msimu huu lakini hiyo ni aibu kwa Simba.
“Binafsi naona Maguli anafanya vyema, anastahili kupongezwa lakini hiyo ni salamu
tosha kwa Simba na inaonyesha kitendo cha kumuacha hakikuwa cha kiungwana kwa sababu uwezo
alikuwa nao lakini ndiyo hivyo, wakamfungashia virago kama ilivyokuwa kwangu.
“Zaidi anatakiwa kujituma kwa bidii na kuendelea
hivyo bila kubweteka, soka ni popote, cha msingi ni kujituma tu.Kwa sasa mimi
binafasi naendelea kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mwadui FC,
ushindani umekuwa mkubwa kwenye ligi,” alisema Tambwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment