Tamasha la
Majimaji Selebuka limepangwa kufanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 17 mjini Songea.
“Tamasha
litajumuisha mambo muhimu, kutakuwa na michezo ya mbio za baiskeli, pia
marathoni na tayari kuna wanariadha kutoka nchi jirani wamejitokeza kushiriki,”
alisema.
“Pia
tutakuwa na maonyesho ya kitamaduni, masuala ya utalii na wageni mbalimbali
kutoka ndani na nje ya Tanzania wameanza kuwasili,” alisema.
“Lengo la
kufanya hivi ni kutambua juhudi za shughuli za kiuchumi za wajasiriamali wa
mkoa wa Ruvuma kupitia maonyesho ya shughuli za wajasiriamali wadogo.”
Tamasha
linalenga pia kupanua soko la wajasiriamali hao kwa watu tofauti kwani kutakuwa
na wageni mbali mbali walioalikwa toka ndani na nje ya nchi.
0 COMMENTS:
Post a Comment