October 9, 2015

DK MAGUFULI AKIWA NA MMOJA WA WAGOMBEA UBUNGE WA CCM, FREDERICK MWAKALEBELA ALIYEWAHI KUWA KATIBU MKUU WA TFF NA MTENDAJI WA MTIBWA SUGAR. 

Na Richard Bukos, Kilimanjaro
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Pombe Magufuli, juzi Jumatano alisitisha kwa muda kampeni zake za kuomba kura na kuanza kutangaza matokeo ya mechi ya Taifa Stars iliyokuwa inaongoza dhidi ya Malawi mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.


Kampeni hizo zilifanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa uliopo Moshi Mjini ambapo zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mchezo huo kumalizika, Magufuli aliutangazia umati uliofurika uwanjani hapo kuwa amefurahishwa na matokeo ya mechi ya Stars katika mchezo huo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018.

“Ndugu zangu Watanzania wenzangu, hivi tunavyoongea nimepata taarifa za faraja sana kutoka Uwanja wa Taifa jijini Dar baada ya kuambiwa mpaka muda huu zikiwa zimesalia dakika chache mpira kuisha, timu yetu ya taifa, inaongoza kwa mabao mawili kwa bila.

“Hilo ni jambo la faraja sana kwani matokeo hayo yamenifurahisha sana na kama nilivyosema katika kampeni zangu kuwa nitafanya kila niwezavyo ili niinue soka la hapa nchini ikiwemo timu ya taifa,” alisema Magufuli.


Mara baada ya kauli hiyo ya Magufuli ambaye alijinadi kuwa enzi zake alikuwa kipa, alipata shangwe kubwa.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Unatumika tu, huyu jamaa hajawahi kuwa mwanamichezo na alishawahi kukili hilo!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic