Kocha
Msaidizi wa timu ya taifa ya vijana chini miaka 23, Shaun Bartlett ameeleza jambo la kiufundi ambalo
Taifa Stars walikosea na kuruhusu Algeria kurudisha mabao yote mawili.
Bartlett
ameiambia SALEHJEMBE, kwamba Algeria walitumia mfumo wa kupiga mipira nyuma ya
mabeki wa Stars ambao umekuwa ukiwasumbua wengi.
“Soka
linakwenda linabadilika, kila kitu kinakuwa tofauti. Hata beki anavyosimama
sasa inakuwa ni tofauti.
“Nimeona
mabeki wa Tanzania hawakuwa tayari katika kupambana na mfumo huo. Sayansi
inasema hivi, unapokuwa unaangalia upande wa lango la upinzani.
“Halafu
mchezaji wa timu pinzani anaangalia upande wa lango lako, ukapigwa mpira kwenda
kwenye lango lako, yeye ndiye anakuwa na nafasi zaidi ya kufanya vizuri.
“Algeria
walilitumia hilo, utaona mabeki wa Tanzania hawakujua ndiyo maana kila
walipokuwa wanageuka wanakuta tayari mchezaji wa Algeria ana mpira na madhara
yapo kwenye lango lao,” alisema Bartlett.
“Kupambana
na hilo, lazima mabeki wanatakiwa kusimama nusu, wakiangalia pembeni ya uwanja
ili iwe lahisi kugeuka na kukimbia kama mpira utapigwa nyuma yao”
Bartlett
amesisitiza Stars bado ina nafasi hata kama inacheza ugenini leo dhidi ya
Algeria. Inategemea itacheza kwa mipango na nidhamu ipi.
Kikosi cha Barltett kiliifunga Stars kwa mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Eldorado jijini Johannesburg, Afrika Kusini wiki moja iliyopita wakati Stars ikiwa kambini nchini humo kujiandaa na mechi hiyo dhidi ya Algeria.
0 COMMENTS:
Post a Comment