November 17, 2015


Kamati ya Taifa Stars kupitia Mwenyekiti wake, Farouk Baghoza imetoa kitita cha SH milioni 25 kwa wachezaji wa Taifa Stars baada ya sare ya bao 2-2 dhidi ya Algeria.

Awali kamati hiyo iliahidi kitita cha Sh milioni 50 kama ingeishinda Algeria. Lakini ikaambulia sare ya bao 2-2.

Lakini sasa kuna ahadi ya Sh milioni 500 ambayo imetolewa kama Stars itashinda au kupata sare itakayoivusha Stars hadi hatua ya makundi.

Stars inatakiwa kushinda au sare ya kuanzia bao 3-3 ili iweze kusonga mbele.


Tayari kikosi cha Stars iko mjini Bilda, Algeria kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic