Inaonekana beki raia wa Togo,Vincent Bossou amepania kuichukua nafasi ya nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro'
Kurejea kwa beki huyo, huenda kukawa kikwazo
kwa mabeki wa kati wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani
kwenye kikosi hicho kinachopigana kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Mtogo huyo, tangu atue Yanga amekuwa hapati
nafasi ya uhakika ya kucheza katika kikosi cha kwanza kinachonolewa na Mholanzi,
Hans van Der Pluijm.
Beki huyo, jana asubuhi alijitahidi kumshawishi
Pluijm wakati Yanga ilipocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Makongo Academy
kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 3-0
yaliyofungwa na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ kwa penalti, Franky Gerald na
Donald Ngoma, Bossou alicheza kwa kuelewana na Mbuyu Twite na kuzuia hatari
langoni kwao.
Pluijm
amesema kuwa kila siku anajaribu kombinesheni mpya ya wachezaji kwenye kikosi
chake, na Bossou na Twite wamemfurahisha.
Pluijm alisema: “Nafurahia kuona mabadiliko ya
Bossou kadiri siku zinavyokwenda kuanzia mazoezini hadi kwenye baadhi ya mechi
anazocheza, hakuna mchezaji mwenye nafasi ya kudumu hapa, huyu akiendelea hivi
atapata nafasi kikosini.”







0 COMMENTS:
Post a Comment