November 28, 2015


Bahati hufuata bahati! Unaweza kusema hivyo lakini ukweli utendaji wa kazi wa juhudi, unalipa.


Maana Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe, mambo yamekuwa yakizidi kumnyookea  sasa timu kutoka nchini Uswiss nayo inamtaka akafanye majaribio.

Timu hiyo ya Uswiss imeibuka ikiwa ni siku chache tu baada ya moja ya timu tajiri nchini Afrika Kusini ya Mamelodi Sundown kuonyesha nia ya kumpata.

Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amesema :

“Hiyo klabu ya Uswisi inayomtaka Ngoma ni ya Ligi Kuu Uswisi, hii ndiyo iliyokuwa ya kwanza kumhitaji straika huyu lakini nimekuwa nikisikia pia taarifa za Mamelodi ingawa hazijafiga klabu rasmi."

Hata hivyo, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ameshasisitiza kutokuwa tayari kumuachia Ngoma aondoke kikosini mwake kwani ana mpango naye wa muda mrefu katika michuano ya kimataifa.


“Tuna ligi kuu, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya, unamuachiaje mtu kama Ngoma kwa wakati huu? Ngoma haondoki na sitakuwa tayari kumuachia jueni hivyo,” alisema Pluijm, raia wa Uholanzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic